
- Asema Serikali imedhamiria kulifanya Soko la Madini Dar es salaam kuwa Kama Dubai.
- Aeleza namna Serikali itaweka mazingira Bora na wezeshi ya Biashara ya madini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Serikali imedhamiria kukuza na kuboresha Soko la Madini Dar es salaam kwa kulifanya kuwa la Kisasa zaidi ili kuvutia wateja wa ndani na Nje ya Nchi hali itakayowezesha Serikali kupata Kodi na Wafanyabiashara kunufaika.
RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao Cha Wadau wa madini ambapo amesema Dar es salaam ina kila sababu ya kuwa Soko kubwa la Madini Kama ilivyo Dubai.
Aidha RC Makalla amesema tangu kuanzishwa kwa Soko la Madini Dar es salaam biashara zenye thamani ya Shilingi bilioni 23.6 zimefanyika na kuwezesha Serikali kupata Kodi isiyopungua Shilingi bilioni 1.6.
Hata hivyo RC Makalla amesema uwepo wa Soko Hilo umesaidia kupungua kwa Vitendo ya Wizi na utapeli wa madini na kukuza Imani kwa wanunuzi wa ndani na Nje ya Nchi.

Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza wote waliopewa vibali vya kuchimba mchanga, Vifusi na Kokoto kufanya jukumu hilo kwa kufuata sheria na miongozo ikiwa ni pamoja na kushirikisha wakazi wa eneo husika.
Kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili Wadau wa madini, RC Makalla ameahidi kuzitatua kwa kushirikisha Wizara husika.
No comments:
Post a Comment