Monday, November 8, 2021

ELIMU YA FEDHA KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja, akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliwakaribisha wananchi kuhudhuria maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yatakayofanyika kwa siku 7.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja, akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa wito kwa wananchi kufika katika maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yatakayofanyika kwa siku 7 ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo na riba zake.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja akizungumza na Bi. Mwanahamisi Mketo mmoja wa wajasiliamali kutoka kikundi cha Uwazi Makangarawe waliowezeshwa na TASAF alipotembelea mabanda mbalimbali yaliyoshiriki maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja akipokelewa na Kamishana Msaidizi wa Idara hiyo Bi. Dionisia Mjema alipowasili kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda akitoa maelezo kwa Bw. Jafet Mzava alipotembelea banda la wizara hiyo kwenye maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, akimwongoza Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja (katikati), kutembelea mabanda ya walioshiriki maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishana Msaidizi wa Idara hiyo Bi. Deoninsia Mjema.
Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dar es Salaam | Kamishna wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini, Dkt. Charles Mwamwaja amesema kuwa watanzania chini ya asilimia 50 ndio waliofikiwa na huduma za fedha jambo ambalo limeifanya Serikali kuwa na Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ili kuongeza uelewa kwa wananchi kwa lengo la kuchochea ustawi wa jamii.
Hayo ameyabainisha wakati akitembelea mabanda katika maonesho ya Wiki ya Fedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ya kwanza ya maonesho hayo.
Alisema huduma za fedha zinarahisisha utaratibu wa kubadilishana bidhaa na huduma jambo ambalo ni muhimu katika maendeleo ya uchumi kwa nchi yeyote Duniani ikiwemo Tanzania hivyo ni lazima kuwa na mkakati wa kutoa elimu kwa umma kuhusu uelewa wa huduma hiyo.
“Watu wanadhulumiwa na hawajui waende wapi, nani ni mtoaji wa huduma hiyo rasmi, mteja akidhulumiwa aende wapi na hawajui kuwa mteja wa huduma za fedha analindwa, hivyo Serikali imeamua kutoa elimu kwa umma ili kuondoa sintofahamu hiyo”. alieleza Dkt. Mwamwaja
Dkt. Mwamwaja alisema kuwa Sekta ya Fedha inarahisisha upatikanaji wa mitaji na uwekezaji ndio maana vikundi vidogo vya kuweka na kukopa kama Vikoba, vinasaidia kukuza mitaji ambayo inaweza kutumika kuwekeza kwenye miradi ya ufugaji na mingine ambayo inamanufaa si tu kwa mtu mmoja mmoja bali kwa Taifa kwa ujumla.
Aidha alisema matokeo chanya ya Sekta ya Fedha hayawezi kufikiwa bila kuwekeza katika elimu ili wananchi waweze kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao na nchi kwa ujumla.
Vilevile Dkt. Mwamwaja alisema umbo la Sekta ya Fedha limegawanyika katika maeneo matano ambayo ni masuala yanayohusiana na huduma za Benki, Bima, Masoko ya Mitaji na Dhamana, Mifuko ya Jamii na Huduma ndogo ya Fedha.
Maonesho ya Huduma za Fedha Kitaifa yameanza Novemba 8 na kutarajiwa kuhitimishwa Novemba 14 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
TARATIBU ZA URASIMISHAJI WA BIASHARA KWA KUSAJILI NA KUTOA LESENI ZA BIASHARA NA VIWANDA KWA NJIA YA MTANDAO KUPITIA BRELA ZIMESAIDIA KUVUTIA WAWEKEZAJI: MHE. KIGAHE
Older Article
MAHAKAMA SPORTS YANYAKUA VIKOMBE VITATU MASHINDANO YA SHIMIWI
Absa Group Reports 10% Increase in 2024 Earnings after Material Second-Half Recovery
Hassani MakeroMar 11, 2025Benki ya NBC Yaandaa Hafla ya Futari Zanzibar, Yajivunia Ongezeko la Wateja
Hassani MakeroMar 07, 2025BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA RASHAL ENERGIES, INAYOJENGA BOMBA LA GESI KISEMVULE-MBAGALA
Hassani MakeroMar 07, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment