AWESO ATATUA CHANGAMOTO YA MAJI YA 'FLOURIDE' WILAYANI ARUMERU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, February 27, 2022

AWESO ATATUA CHANGAMOTO YA MAJI YA 'FLOURIDE' WILAYANI ARUMERU

Waziri wa maji Jumaa Aweso akizungumza na wadau wa maji katika hafla ya makabidhiano ya kituo cha ubora wa maji eneo la Ngurdoto Wilayani Arumeru.
Waziri wa maji Jumaa Aweso akipokea ripoti ya kituo cha utafiti wa ubora wa maji mara baada ya kuzungumza na wadau wa maji.
Wadau wa maji wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiongozwa na Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jiji la Arusha mhandisi Jastine Rujomba.


Na Jane Edward, Arumeru | Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa sh,milioni 100 kwaajili ya kuboresha mradi wa utafiti wa ubora wa maji aina ya Flouride uliopo Ngurdoto Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Ambapo ameagiza vituo vya utafiti wa maji viendelezwe ili kuzalisha wataalam na changamoto zinazoikumba sekta ya maji hivyo ni lazima kufanya tafiti zaidi na kubaini aina za dawa zinazochanganywa zinatoka ndani ya nchi na si kuziagiza nje ya nchi ili serikali iweze kuondokana na changamoto za maji.

Aweso ametoa fedha hizo kupitia Wizara ya Maji katika halfa ya makabidhiano ya kituo cha Ngurdoto kwa Chuo cha Maji chini ya Wizara ya Maji.

Amesema wizara imetoa fedha hizo kwa kituo hicho kwaajili ya kufanya tafiti na kutoa majawabu kwa wizara ya maji katika kutatua changamoto ya madini ya floride yanayotesa wananchi.

Amebainisha kuwa wizara hiyo inataka kuona kituo hicho kiwe bora zaidi na haiwezekani watu wanachukua sampuli za maji na kwenda kupima maeneo mengine huku wakikiacha kituo hicho kikiwa kinashindwa kufanya kazi.

Amesema kituo hicho kinatakiwa kuwa kimbilio kwa wananchi wanaohitaji kufanyiwa tafiti za changamoto zinazoikumba sekta ya maji na ndio maana Mamlaka za maji zitumie dawa zake ili kuruhusu wananchi wapate maji hivyo lazima vituo vya utafiti kutokuwa na haja ya kuagiza madawa nje ya nchi badala yake watumie dawa za ndani ya nchi.

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Kituo hicho cha Utafiti,Masumbuko Msongo alisema kituo hicho kinatumia teknolojia ya chenga za Mkaa unaotokana na mifupa ya ng'ombe na kuondoa madini ya fluoride.

Amesema hadi sasa mitambo 1,735 ya ngazi ya kaya imetengenezwa na kusambazwa katika mikoa ya Manyara ambapo wananchi 13,880 wamenufaika na teknolojia lakini wanakabiliwa na changamoto kutumia tanuru zinazotengenezwa na matofali ya china ambazo husinyaa baada ya kutumika.

Ambapo kukosekana kwa vifaa vya kisasa vya kimaabara kumefanya kituo hicho kutofikia malengo ya kukuza teknolojia nyingine zinazotumia malighafi zinazopatikana.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango alisema wakazi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya madini ya Floride yenye kuharibu viungo vya mwili na wengine kupata ulemavu wa viungo mbalimbali.

Amesema uwepo wa kituo hicho kitawanufaisha wananchi mbalimbali wanaokumbana na changamoto za maji katika vijiji 157 vilivyopo wilayani humo.

Huku Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, John Pallangyo alisema licha ya wilaya hiyo kuwa na vyanzo vingi vya maji lakini bado wananchi hawana maji na wengine wakipata maji yenye florida huku akiomba wananchi wa Kata za Mbuguni, Kikwe, Makiba na Shambarai Burka wakiwa hawana uhakika wa upatikanaji wa maji safi na salama na wanahofu ya kupata maji sababu ni muda mrefu hawajapata maji.

Wakati huo huo,Makamu wa Chuo Kikuu cha Arusha (Arusha University), Profesa, Patrick Manu alisema kituo hicho cha utafiti wa ubora wa maji walitoa eneo hilo bure kwa serikali na kutoa ombi kwa wizara ya maji kupata maji safi na salama kwani hivi sasa chuo hicho kinanunua maji safi na salama nje ya chuo kwasababu maji yanayotoka chuoni hapo yana floride nyingi na hayafai kutumika kwa binadamu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages