SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, February 24, 2022

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Vuga Mjini Zanzibar,leo Februari 24, 2022.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.Tulia Ackson (Mb), katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Vuga Mjini Zanzibar,leo Februari 24, 2022.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.Tulia Ackson (Mb), akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ofisi za Makamu wa Rais zilizopo Vuga Mjini Zanzibar, Februari 24, 2022

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson kwa jitihada anayoendelea kuionesha katika kuliongoza Bunge kwa maslahi ya Taifa.

Mhe. Hemed Ametoa kauli hio alipofanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson alipofika kujitambulisha kwa mara ya kwanza tokea achaguliwe kushika nyadhifa hiyo Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Mhe Hemed amesema Serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ina Imani kubwa sana na utendaji kazi wake ndani na nje ya Bunge anaoendelea kuionyesha kwa maslahi ya Watanzania.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuhakikishia Spika huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi itatoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanishi na kuweza kuwaletea maendeleo wananchi wa taifa hili.

Mhe Hemed amesema kuwa Muhimili wa Bunge ni muhimu ambao una uwakilishi wa watanzania wote hivyo ana Imani Muhimili huo utasimamia Kanuni na Sheria zilizopo ili kulinda maslahi ya wananchi.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema kuwa kwa ushirikiano uliopo baina ya Spika huyo na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bunge litabaki kuwa salama na kuweza kufikia lengo la Serikali la kuwatumikia wananchi kupitia Wabunge hao liweze kufikiwa.

Kwa upende wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Bunge analoliongoza lina mashirikiano ya karibu na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ili kuwaletea maendeleo Wananchi ya Tanzania

Dkt Tulia amesema kuwa Bunge lipo tayari kupokea maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi ili kufikia malengo waliojipangia ya kuwahudumia wananchi walio wachagua ambao wana matumaini makubwa kupitia chombo hicho cha kutunga na kubadilisha Sheria kwa maslahi yawatanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages