MASHABIKI 35,000 KUSHUHUDIA MTANANGE SIMBA SC VS US GENDARMARIE KWA MKAPA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, March 28, 2022

MASHABIKI 35,000 KUSHUHUDIA MTANANGE SIMBA SC VS US GENDARMARIE KWA MKAPA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeruhusiwa kuingiza mashabiki takribani 35,000 kwenye mchezo wake wa nyumbani wakiwakaribisha timu ya US Gendarmerie mchezo ambao utapigwa tarehe 03/03/2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Simba Sc, Bw.Ahmed Ally amesema tiketi tayari zinauzwa mitandaoni na kwa mashabiki wetu waliopo mikoani hakuna haja ya kununua tiketi hadi wakifika Dar es Salaam.

Tumeruhusiwa mashabiki 35,000. Awali tuliomba kuongeza idadi ya mashabiki kupitia kwa TFF lakini kwa sababu ya mambo ya Covid wameruhusu idadi ya mashabiki 35,000. Mashabiki ambao wanataka kuja kuona mchezo wanunue tiketi mapema.” Amesema Bw.Ahmed Ally.

Amesema wataingia kwenye mchezo wa jumapili wakiwa na lengo moja ushindi na wanaimani watashinda na kutinga hatua ya robo fainali.

Aidha amesema siku ya jumatano watakuwa standi ya Magufuli watakuwa pale kwa pamoja na mgeni wetu rasmi atakuwa ni Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu.

Tukio letu la jumatano kwenye stendi ya Magufuli itakuwa saa 4 hadi 5 asubuhi. Tunakutana pale kufurahi, kushangilia Simba yetu”. Amesema Ahmed Ally.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages