
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Profesa Honest Ngowi pamoja na Dereva wake wamefariki dunia katika ajali ya barararani iliyohusisha magari matatu eneo la Mlandizi Madafu mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamanda ACP Pius Lutumo, amethibitisha.
Kamanda Lutumo akiwa eneo la tulio amesema magari hayo matatu ni Noah, Land Cruiser na Lori la kontena ambalo amesema lilikuwa likitokea Morogoro na Kahama njia na kwanza kuikwaruza ubavuni hiyo Noah kabla ya kuserereka na kontena lake kuanguka na kuilalia LandCruiser alilokuwamo Profesa Ngowi na Dereva.
Amesema dereva alifariki hapo hapo wakati Profesa Ngowi alifia hospitali alikokimbizwa baada ya kutolewa akiwa hai lakini majeruhi.
Marehemu Profesa Ngowi atakumbukwa pia kama mtangazaji mahiri wa vipindi vya Uchumi ITV.
"Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine, taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu, Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito" Ofisi ya Mawasiliano Mzumbe.

MOLA AIPUMZISHE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI - AMINA

No comments:
Post a Comment