MWAMOTO AKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, March 3, 2022

MWAMOTO AKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa Mbunge wa wa Jimbo la Kilolo Mkoani Iringa Venance Mwamoto amemwagia sifa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi bora na tija kwa Taifa.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwamoto amesema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia, Tanzania imeshuhudiwa ikifanya mambo makubwa na yenye maendeleo tofauti na watu wengi walivyotarajia.

Akitolea mfano wa ujenzi wa madarasa, zahanati, hospitali, miundombinu ya treni ya kisasa(SGR), Daraja la Tanzanite, bwawa la kufua umeme le Nyerere pamoja na ajira kwa makundi mbalimbali, Mwamoto alisema hayo na mengine yote ni mfano wa kiongozi bora anayejali maisha ya wananchi wake.

"Amegusa maisha ya watanzania wengi kuanzia ngazi ya chini, hivi sasa ukienda vijijini wananchi wana furaha kubwa hasa kutokana na ujenzi wa madarasa na shule, ukweli ndani ya kipindi hiki anachoelekea kutimiza mwaka mmoja ' kaupiga mwingi' alisema Mwamoto.

Aidha amesema mikutano mbalimbali ya kimataifa aliyoshiriki Rais Samia Suluhu Hassan ni kielelezo tosha na kupenda ushirikiano wa kidiplomasia huku akiwataka watanzania kuendelea kumuunga mkono wakati huu ambapo anaendelea kuijenga nchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages