NGAIZA FOUNDATION WASIMAMA NA RAIS SAMIA KUPIGANIA ELIMU BORA KWA MTOTO WA KIKE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, March 1, 2022

NGAIZA FOUNDATION WASIMAMA NA RAIS SAMIA KUPIGANIA ELIMU BORA KWA MTOTO WA KIKE

  • Wampongeza kwa uamuzi wa kuruhusu waliopata ujauzito kurejea shuleni.
  • Wasema Kampeni ya NIACHE NISOME imekuwa na mafanikio makubwa kwa watoto wa kike.
Shirika lisilo la Kiserikali la NGAIZA FOUNDATION limesema litaendelea kushirikiana na Rais SAMIA SULUHU HASSAN katika jitiada anazofanya kuboresha suala la Elimu hususani kwa mtoto wa kike ambapo limesema uamuzi wake wa kuruhusu Wanafunzi wa kike waliokuwa wamepata ujauzito kurejea shuleni ulikuwa na tija kubwa Sana katika kumkwamua mwanamke.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bi. ELIZABETH NGAIZA amesema katika kuelekea siku ya Wanawake Duniani March 08, Wanawake tunajivunia kupata Rais Shupavu mwanamke ambae licha ya kuliongoza vizuri Taifa pia ameonyesha dhamira ya dhati kumkwamua Mtoto wa kike hususani pale alipotangaza kuruhusu Wanafunzi wa kike waliopata ujauzito kurejea shuleni.

Kutokana na hilo Bi. NGAIZA ametoa wito kwa Wananchi na Wanawake nchini kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ili aweze kutimiza maono makubwa na mapana aliyoyabeba kwa maslahi ya Taifa.

Aidha Bi. NGAIZA amesema kwakuwa sheria ipo na inafanya kazi ni vyema wanaohusika kuwapa ujauzito Wanafunzi wakaendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ili iwe fundisho huku akiwataka Wazazi kuacha tabia ya kumaliza masuala hayo kifamilia.

Hata hivyo NGAIZA amesema katika Kampeni ya NIACHE NISOME inayolenga kupambania usawa wa Elimu kwa mtoto wa kike inayoendeshwa na shirika hilo wamekutana na Kilio Cha Wazazi wanaolalamikia kutozwa fedha za ununuzi wa Madawati licha ya Serikali kununua Madawati ambapo wameiomba Serikali kulitazama suala hilo.
Itakumbukwa kuwa Rais Samia alisema suala la kurudi shule haliwahusu wanafunzi waliopata mimba pekee bali wanafunzi wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro, ujauzito na nidhamu ili kutoa fursa kwa watoto wa Tanzania kupata elimu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages