KAFULILA AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA VYAMA VYA USHIRIKA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Wednesday, April 20, 2022

demo-image

KAFULILA AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA VYAMA VYA USHIRIKA

IMG-20220420-WA0058
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila akiongea na wadau wa zao la Pamba mkoani Simiyu.

Na Costatine Mathias, Simiyu

MKUU wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ameitaka Taasisi ya Kupambana na Kuziua Rushwa Mkoani humo kuhakikisha wanakamilisha uchunguzi juu vyama vya ushirika ambavyo vilipokea fedha na kuwalipa wakulima ili kujiridhisha kama malipo hayo ni sahihi.

Kafulila ameyasema hayo leo (Aprili 20,2022) kwenye mkutano wa kujadili tathimini ya zao la pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Bariadi Conference na kuwakutanisha wadau wa pamba mkoani humo.

‘’Nataka nione kama Amcos zimewalipa wakulima kulingana na fedha walizopokea toka kwenye makampuni ya ununuzi wa pamba, tusiache jiwe juu ya jiwe, tusiache mtu hata mmoja aliyekula fedha za mkulima’’, amesema Kafulila.

Hata hivyo Kafulila ameshangazwa kuona Taasisi hiyo haijafanya uchunguzi tangu alipotoa maagizo jambo ambalo amesema limesikitisha sana, na kwamba ameitaka TAKUKURU kufanya uchunguzi huo haraka na aipate ripoti hiyo.

Aidha Kafulila amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya Ushirika bado wanawaibia wakulima kupitia vyama vya ushirika ambapo si lengo la serikali kuwaibia wakulima kupitia ushirika.

‘’Tunataka kuona Mnunuzi hamwibii mkulima, Mkulima anataka bei stahiki na mnunuzi anataka kutoa bei stahiki…’’ amesema Kafulila.

Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amesema mkoa wa Simiyu ndio wazalishaji wakubwa wa pamba nchini na kwamba changamoto nyingi za zao la pamba ziko mkoa wa Simiyu.

Alisema viongozi wa Amcos hawaambii wakulima juu ya mabadiliko ya bei, wanalipwa fedha kidogo wakati makampuni yanatoa bei kubwa kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *