RC MAKALLA: MRADI WA MAJI JIMBO LA KIBAMBA KUKAMILIKA AUGUST MWAKA HUU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, April 27, 2022

RC MAKALLA: MRADI WA MAJI JIMBO LA KIBAMBA KUKAMILIKA AUGUST MWAKA HUU

  • Amshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha Za uviko Bilioni 2:5 Na maekekezo makusudi ya kutatua kero ya Maji Jimbo la Kibamba.
  • Ampongeza Mbunge Mtemvu kwa ufuatiliaji wa mradi huu tangu akiwa diwani.
  • Awapongeza DAWASA kwa kazi Nzuri ya utekelezaji miradi mingi kwa ufanisi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Mradi wa Maji wa Mshikamano Jimbo la Kibamba unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi August Mwaka huu ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha za UVIKO19 kiasi Cha Shilingi Bilioni 2.5 kutatua kero ya Maji Jimbo la Kibamba.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Miradi huo,RC Makalla amesema Mradi huo unagharimu Shilingi Bilioni 4.8 ikiwa ni Bilioni 2.5 za UVIKO19 na kiasi kilichobaki ni mapato ya ndani ya DAWASA ukihusisha Ujenzi wa Tank la Lita Milioni 6, Ulazaji wa Mabomba na Kituo Cha kusukuma Maji.

Aidha RC Makalla amemuelekeza Mkandarasi kuongeza bidii ili kuhakikisha Ujenzi unakamilika kabla ya Mwezi August Mwaka huu ambapo mpaka Sasa Mradi upo Asilimia 30.
Pamoja na hayo RC Makalla amewasifu na kuwapongeza DAWASA kwa kazi kubwa na nzuri ya utekelezaji wa miradi mingi ya Maji kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages