PWANI YA BAGAMOYO!

Wachuuzi wa samaki wakiandaa biashara zao eneo la pwani ya bahari ya Hindi katika Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani, Aprili 14, 2022. Shughuli za uvuvi, biashara ya samaki na mazao mengine ya bahari ni moja ya njia muhimu za kujipatia riziki kwa wakazi wengi wa mji huo wengine wakitegemea kilimo na ufugaji. Ikiwa umbali wa kilomita 75 kaskazini ya Mji wa Dar es Salaam na Kilomita 45 magharibi mwa Kisiwa cha Unguja, Mji wa Bagamoyo umesheni historia lukuki za kale zinazoufanya Bagamoyo kuwa na vivutio vya aina yake vya utalii ambapo pia endapo mamlaka zinazohusika zikibariki kufanyika kwa mradi wa uwekezaji wa ukanda maalumu wa Bagamoyo mchakato utakapokamilika zitasaidia kuinua uchumi wa Bagamoyo na wakazi wake. (Photo: PETER MGONGO)
No comments:
Post a Comment