MASAUNI ATOA MAAGIZO KWA JESHI LA POLISI, WAPEWA SIKU SABA KUKAMATA 'PANYA ROAD' - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, May 3, 2022

MASAUNI ATOA MAAGIZO KWA JESHI LA POLISI, WAPEWA SIKU SABA KUKAMATA 'PANYA ROAD'

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni akizungumza leo Mei 3, 2022 na wakazi wa kata ya Gogo, Zingiziwa na Chanika kuhusiana na 'Panya Road' wanaovunja na kujeruhi wananchi, kuvunja na kuiba katika maeneo malimbali ya wakazi wa maeneo hayo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro akizungumza na akizungumza leo Mei 3, 2022 na wakazi wa kata ya Gogo, Zingiziwa na Chanika jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, kuhusiana na 'Panya Road' wanaovunja na kujeruhi wananchi, kuvunja na kuiba katika maeneo malimbali ya wakazi wa maeneo hayo.
Baadhi ya wananchi wa maeneo ya kata ya Gogo, Zingiziwa na Chanika jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, waliojeruhiwa na 'Panya Road' wakiwa kwenye Mkutano wa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni alipofika katika maeneo hayo leo Mei 3, 2022.
Moja ya wananchi wa maeneo ya kata ya Gogo, Zingiziwa na Chanika jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, wakitoa maoni juu ya 'Panya Road' kwenye Mkutano wa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni alipofika katika maeneo hayo leo Mei 3, 2022.
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni akiwajulia hali majeruhi waliojeruhiwa na 'Panya Road' alipofika katika maeneo hayo leo Mei 3, 2022.
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamadi Masauni akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro na Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro walipotembelea Kata ya Chanika, Gogo na Zingiziwa leo Mei 3, 2022.

WAZIRI wa Mambo ya ndani, Hamad Masauni atoa maagizo kwa jeshi la polisi kuwakamata vijana wanaodhaniwa kuwa ni 'Panya Road' katika kata ya Zingiziwa, Gogo na Chanika jijini Dar es Salaam.

Amewapa siku saba Jeshi la Polisi nchini kuwakamata vijana wanaodhaniwa kuwa ni 'Panya road' na kuwaasa wazazi kuwa ndio walinzi namba moja juu ya watoto wao na katika amilia zao.

Licha ya hayo Mhandisi Masauni amewaasa wananchi wa Jimbo la Ukonga kuwa na ulinzi shirikishi katika maeneo yao. Amewaasa wananchi wa Kata hizo kuwa na ushirikiano na Jeshi la polisi katika eneo hilo ili kudhibiti uharifu unaoendelea katika maeneo ya

Ameyasema hayo leo Mei 3, 2022 alipotembelea katika kata hizo, amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na vijana hao havikubaliki kabisa katika jamii.

Aprili, 24, 2022 Jimbo la Ukonga, kata ya Chanika, Gogo na Zingiziwa kuliibuka na 'Panya road' waliojeruhi wananchi kwa mapanga, Kuvunja na Kuiba vitu mbalimbali majumbani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages