RC MAKALLA: OPERESHENI IMEDHIBITI MATUKIO YA PANYA ROAD DSM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, May 18, 2022

RC MAKALLA: OPERESHENI IMEDHIBITI MATUKIO YA PANYA ROAD DSM

- Asema Tangu opersheni ianze Mkoa upo Shwari.

- Apongeza Jeshi la Polisi kwa kuwashughulikia kikamilifu Panya road.

- Watuhumiwa 35 wamefikiahwa Mahakamani, 17 Uchunguzi unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema kwa Sasa Mkoa upo Shwari kufuata Operesheni kabambe ya kuwakamata Panya road waliokuwa wakifanya matukio ya uhalifi maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

RC Makalla amesema Mpaka Sasa Operesheni imefanikiwa kuwafikisha Mahakama Watuhumiwa 35 na wengine 17 wanaendelea kufanyiwa Uchunguzi.

Kutokana na Hilo RC Makalla amewatoa hofu Wananchi wa Mkoa huo na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuvunja Uti wa mgongo wa mtandao mzima wa Panya road.

Ili kuhakikisha matukio Kama hayo hayajirudii Mara kwa Mara, RC Makalla amesema wameweka Mpango mkakati endelevu kwa kudhibiti uhalifu wa Aina yoyote usitokee kwenye Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages