TANAPA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA KENYA WILDLIFE SERVICE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, June 11, 2022

TANAPA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA KENYA WILDLIFE SERVICE


Na Emil Ngowi, ARUSHA

Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Herman Batiho anayesimamia Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara – TANAPA, jana alipokea ugeni toka KWS na kusisitiza kuwa ushirikiano baina ya Kenya na Tanzania ni muhimu katika kuhakikisha wanyama wetu wanalindwa kikamilifu hivyo kuona kuwa kuna haja kubwa kuwa na mpango wa uhifadhi wa wanyama pori katika mipaka ya Kenya na Tanzania .

Kikao hiki kimefanyika makao makuu ya TANAPA jana, kati ya Kenya Wildlife Service (KWS) na TANAPA.

Akiwasilisha baadhi ya changamoto za uhifadhi katika mipaka, Afisa Uhifadhi Mwandamizi Emmanuel Kaaya alisema “kutokuwa na makubaliano ya pamoja kati ya Tanzania na Kenya ya namna ya kuwahifadhi wanyama mpakani kumesababisha wanyama kuhesabiwa mara mbili wakati wa zoezi la sensa ya wanyama.”

Ujumbe kutoka KWS uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Brig. John Waweru akiambatana na Mkurugenzi wa WRTI, Dkt. Patrick Omondi pamoja na watumishi wengine wa KWS.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages