
Mratibu wa World Vision mradi wa Mnyuzi ADP, Samuel Charles akimkabidhi zawadi ya begi mmoja wa wanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa darasa la nne Wilayani korogwe mkoani Tanga.

Mratibu wa World Vision (WVT) mradi wa Mnyuzi ADP Samuel Charles.


Raisa Said, Korogwe
HALMASHAURI ya Wilaya ya Korogwe imesema itawachukulia hatua baadhi ya wazazi wanaowaachisha watoto wao masomo na kuwapeleka kufanya kazi za ndani mijini.
Onyo hilo limetolewa na Afisa Maendleo ya Jamii kaika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe David Mpumiwa kwenye sherehe za kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika ngazi za Wilaya katika Kijiji cha Lusanga katika kata ya Mnyuzi wilayani Korogwe.
Mpumilwa, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED), alisema kuwa kuwaachisha watoto, hasa wasichana masomo na kuwapeleka katika kazi za ndani ni unyanyasaji na kuwanyimwa haki ya watoto kufuata na kufikia ndoto zao za ma isha na kinyume cha sheria.
Mpumilwa ingawa hakutaja idadi ya watoto wa aina hiyo ambao wameachishwa masomo akasema baadhi ya kesi hizo sasa zinashughulikiwa na Jeshi la Polisi. Alisema tu kwamba baadhi ya wazazi walikuwa bado wanaendelea kudumisha tabia hiyo katika eneo hilo.
Alisema inasikitisha kuona tatizo hilo likiendelea katika kata zenye Kamati za Mpango wa Taifa kwa ajili ya kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA).
"Tunawapa wazazi ambao wamesaidia watoto wao kutoroka shuleni kuripoti kwa Maafisa Watendaji wa kata siku ya Jumatatu wakiwa na watoto wao au ama sivyo watachukuliwa hatua za kisheria,” Mpumilwa aliamuru.
Mpumilwa alikemea tabia ya kuwatumia watoto chanzo cha kuwaingizia kipato akisema ajira ya watoto haikubaliki katika aina zake zote.
Mpumilwa aliipongeza shirika la World Vision Tanzania (WVT) kwa kuendeleza programu zinazojihusisha na kuimarisha ulinzi wa watoto ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombini ya afya, elimu na maji.
Ofisa Ustawi wa Jamii katika halmashauri hiyo, Richard Nchimbi alitoa wito jamii kubadilika, akisema kuwa ni aibu kuona mimba za utotoni, utoro ukiendelea pamoja na uwekezaji wote ikifanywa na shirika la World Visiona katika Kata hiyo.
Aidha alikemea tabia ya wazazi kusuluhisha masuala ya unyanyasaji wa watoto nyumbani na kuzuia serikali kuwadhibu wahalifu.
Awali Mratibu wa World Vision WVT mradi wa Mnyuzi ADP, Samuel Charles, alisema kuwa shirika limechukua hatua ya kuanzisha na kuimarisha kamati za MTAKUWA katika vijiji 12 katika kata mbili za Mnyuzi na Kwagunda
Pia wameimarisha na kuanzisha Mabaraza ya watoto katika shule za msingi kwa kushirikiana na serikali ili kuwawezesha watoto kupaza sauti zao dhidi ya unyanyasaji ambao unajulikana kutendwa zaidi na ndugu na jamaa wa karibu wa watoto hao.
Aidha amesema kwenye jamii bado yapo matendo kama ndoa za utotoni,kulazimishwa,mimba za utotoni,ukeketaji na vipigo katika familia hivyo serikali inatakiwa kwa kushirikiana na wadau kupingana na mambo hayo.
Hata hivyo katika maadhimisho hayo shirika hilo la World Vision Tanzania kupitia eneo la Mnyuzi waliweza kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo madaftari na mabegi ya shule Kwa watoto waliofanya vizuri katika mitihani ya darasa la nne .
No comments:
Post a Comment