NIC Shirikianeni Na Taasisi Za Fedha Katika Kutoa Bima Kwa Wakulima-Spika Dkt.Tulia - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, August 5, 2022

NIC Shirikianeni Na Taasisi Za Fedha Katika Kutoa Bima Kwa Wakulima-Spika Dkt.Tulia

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akipata maelezo kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Alex Suzuguye kuhusiana na Bima ya Kilimo pamoja na mifugo alipotembelea Banda la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane 2022 katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson pamoja na Naibu Waziri wa Kilomo Anthony Mavunde wakipokea TiShiti ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) mara baada ya kutembelea banda la NIC kwenye maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane 2022 kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Na Chalila Kibuda, Mbeya

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amesema katika kwenda na teknolojia ya kilimo cha kisasa suala bima ni mhimu kwa wakulima.

Spika Dkt.Tulia ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la shirika la Bima la Taifa (NIC) kwenye maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Amesema kuwa NIC ishirikiane na taasisi za fedha katika kutoa bima kwa wakulima ambapo itakuwa ni dirisha ambalo lina uhakika kukata bima kwenye kilimo.

Dkt.Tulia amesema kilimo kinatakiwa kwenda kisasa kwani bima zitasaidia kuwa na uhakika pindi majanga yakiwafika mkombozi wakulima itakuwa ndio bima.

"Wakulima wakiwa na bima kutafanya kulima kwa uhakika na uzalishaji utaongezeka kwani kupoteza mtaji wake kwenye kilimo anafanya" amesma Dk.Tulia.

Kwenye ziara hiyo Spika Dk.Tulia aliambatana na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde , Mkuu wa Wilaya ya Sogwe Simon Simalenga pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages