RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZAIA KUFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI NA MAKANDA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, September 2, 2023

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZAIA KUFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA WAANDAMIZI NA MAKANDA

SACP DAVID MISIME, Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam

Jeshi la Polisi Nchini limesema linatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa Maafisa wakuu waandamizi kutoka makao makuu na Miko ana vikosi kuanzia septemba 04, 20223 jijini Dae es salaa, kwa lengo la kufanya tathimini ya utendaji kazi katika cha mwaka mmoja.

Akitoa taarifa hiyo leo septemba 02, 20223 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa siku ya Jumatatu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Misime amebainisha kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalam kutoka vyuo vya hapa Nchini na wataalam wa kada mbalimbali ambapo amesema maafisa washiriki watapata fursa ya kufanya tathimini ya majukum ya Jeshi la Polisi na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa mwaka 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia SACP Misime amesema kuwa Mikutano hiyo ni utaratibu wa uliowekwa na Jeshi la Polisi ili kuwakutanisha maafisa wakuu waandamizi Pamoja kufanya tathimini na kuweka mikakati ya kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu hapa Nchini.

Misime ameongeza kuwa Mkuutano huo utaongozwa nakauli mbiu isemayo matumizi ya Tehama kuleta uwazi na ufanisi katika utendaji wa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages