VIFAA VYA USHONI, TEHAMA VYAONGEZA UFANISI BOHARI KUU YA JESHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, October 2, 2023

VIFAA VYA USHONI, TEHAMA VYAONGEZA UFANISI BOHARI KUU YA JESHI

Na Abel Paul, Jeshi la Polisi-Dar es Salaam

Jeshi la Polisi kupitia Bohari kuu imesema imeendelea kusimamia uzalishaji wa sare za maafisa na askari wa Jeshi la Polisi nchini Pamoja na kufunga mifumo ya Tehama na vifaa vya kisasa vya ushoni Bohari kuu ya Jeshi la Polisi.

Akitoa taarifa hiyo leo Octoba 02, 2023 Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Moses Mziray amesema Pamoja na kufanyika maboresho makubwa ndani ya Jeshi hilo Bohari kuu pia imepata vifaa vya kisasa vitakavyowezesha kuongeza uzalishaji wa sare za Jeshi hilo huku akimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa namna ambavyo analiwezesha kiwanda hicho.
ACP Mziray ameongeza kuwa kikosi hicho kimeendelea kushona sare za Jeshi hilo kwa kasi kubwa ambapo amebainisha kuwa mashine hizo zimeongeza ufanisi mkubwa wa utendaji wa kazi kiwandani hapo huku akimshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Camillus Wambura kwa namna ambavyo amewezesha kiwanda hicho kuendelea kuzalisha sare za Maafisa na askari wa Jeshi hilo.
Nae Mkuu wa kiwanda cha ushonaji Bohari kuu ya Jeshi la Polisi Mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Jenitha Mtayoba amesema wanaendelea na ushonaji kwa kasi kubwa kutokana na vifaa vya kisasa vilivyopo kiwandani hapo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages