
Chama cha wafanyakazi wa huduma za Tiba za Dharura Tanzania (EMAT), watendaji na wadau wa Sekta ya Afya Nchini wametakiwa kuchukua jitihada zaidi katika kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili ufahamu na uwelewa juu ya taaluma ya huduma za Afya za dharura iweze kuwafikia wanachi waalio wengi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi ameyasema hayo katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano(5) wa Huduma za Tiba za Dharau uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Jijini Zanzibar.
Amesema wataalamu wa huduma ya Tiba ya Dharura wanapaswa kuwa tayari kutowa Tiba sahihi pale inapohitajika ili kuweza kupata matokeo chanya ya kuokoa maisha pale yanapotokea majanga ya dharura.
Rais Dkt mwinyi amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama nchi zilivyo nchi nyengine Duniani kuwa hatuna kinga ya kutokupata dharura kama vile majanga ya ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani na majanga mbali mbali yanaendelea kupoteza maisha au kuwaachia ulemavu wa kudumu kwa wanachi, hivyo ni lazima kujiandaa kukabiliana na majanaga ya aina yoyote ambayo yanaweza kutokea.
Dkt. Mwinyi amewataka washiriki wa kongamano hilo na wadau wa Sekta ya Afya kuwa tayari katika kuleta ufanisi wa matibabu ya Huduma za Dharura,kwani Serikali zote mbili zimeanzisha Mfumo wa kutoa huduma za Dharura kuanzia Hospital ya Taifa ya Muhimbili na inaendelea kujipanga kuimarisha Mfumo huu katika maeneo yote ya Utoaji huduma za Afya haapa Nchini.

Aidha amesema Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuona umuhimu wa kuwa na Mfumo Imara wa kutowa huduma za Tiba za Dharau katika ngazi zote za utowaji wa huduma za Afya nchini pia imejenga na kuweka vifaa kwenye Idara 119 za Tiba za Dharau hapa Zanzibar Hospitali kumi (10) za Wilaya, na Hospital moja ya Mkoa tayari zinatumia Mfumo wa Tiba ya Dharura.
Sambamba na hayo Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa serikali imeamua kuweka idara ya tiba ya dharura kumi na nne (14) kutoka idara mbili 2 kwaka 2021/2021 lengo ni kuipa kipaombele idara hii ili kupunguza vifo na ulemavu wa kudumu kwa wananchi pindi inapotokea dharura kama vile ajali na nyenginezo.
Nae Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amewataka wanafunzi wanaomaliza masomo yao ya Sekondari kusomea kada ya Huduma ya Tiba za Dharura ambayo imekuwa na uhaba mkubwa wa Madaktari wabobezi wenye uweza wa kutoa huduma za haraka hasa katika kuokoa maisha ya wananchi ambao hupatwa na majanga mbali mabali yasiyotarajiwa.
Amesema kuwa Wizara ya Afya Zanzibar kushirikiana na EMAT wameawaalika wadu tofauti kwa lengo la kubadilisha na uzuefu na taaluma ili kuleta ukuwaji wa haraka wa huduma za dharura na kupata ujuzi na suluhisho za changamoto la ongezeko la vifo vinavyotokana na majanga tofauti.
Kwa upende wake Rais wa Chama cha Wafanyakazi wa Huduma za Tiba za Dharura (EMAT) Dkt. Juma Mfinanga amesema lengo la kongamano la mwaka huu ni kuwaunganisha wataalamu wa tiba ya dharura na ajali kutoka maeneo mbali mbali hapa nchini na nnje ya nchi ili kujadili namna bora ya kuhakikisha huduma za dharura na ajali zinaboreshwa zaidi na kuwa endelevu kwa lengo la kuwafikia wananchi wote bila kujali eneo au uwezo wao wa kifedha.
Amesema kuwa EMAT imejipanga kuhakikisha kuwa na madakatri weledi na wenye Taaluma ya Huduma ya Tiba za Dharura wanafanya kazi ya ziada kuhakikisha vifo vitokanavyo na majangar vinapungua Nchini ambapo kwa sasa asilimia 45 ya vifo vinavyoepukika vimepungua baada ya kuanIshwa kwa EMAT.

Mapema Makamo wapili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt Hussen Ali Mwinyi alikagua mabanda ya maonesho na kupata maelezo ya kitaalamu juu ya utoaji wa Huduma ya Tiba za Dharura yenye mnasaba na Kongamano hilo.

No comments:
Post a Comment