Benki ya Stanbic Tanzania yajipanga kutoa ushirikiano sekta ya nishati ya umeme - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, January 30, 2025

Benki ya Stanbic Tanzania yajipanga kutoa ushirikiano sekta ya nishati ya umeme

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Manzi Rwegasira (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela (kulia), wakati wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika 'Mission 300' uliomalizika hivi karibuni katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Geita Gold Refinery, Bi. Sara Masasi.

Na Jane Edward, Dar es Salaam

Benki ya Stanbic Tanzania imesema inaamini katika upatikanaji wa nishati endelevu yenye tija pamoja na msingi wa ukuai wa uchumi ,ustawi wa jamii,na maendeleo nchini hususani barani Afrika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzii Mtendaji wa Benki hiyo Manzi Rwegasira katika mahojiano maalumu na Michuzi blog wakati wa mkutano wa nishati wa misheni 300 uliomalizika hivi karibuni jijini Dar Es Salaam.

Amesema kuwa benki hiyo imejitokea kuhamasisha upatikanaji wa mitaji,kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ili kutoa suluhisho la fedha katika sekta ya nishati na kusaidia mpango wa mission 300 ili Afrika kupata nishati ya uhakika.

Hata hivyo tanzania imekuwa mmwenyeji wa mkutano wa Marais wa Afrika,wafadhili,taasisi za kifedha na wadau wa maendeleo ili kujadili mikakati ya pamoja na kuwafikishia nishati ya umeme zaidi ya watu milioni 300 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Manzi Rwegasira (wa tatu kutoka kulia), akihudhuria Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika 'Mission 300' uliomalizika hivi karibuni katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages