Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Buyu Zanzibar - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, January 5, 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Buyu Zanzibar

MUONEKANO wa Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, lililowekwa Jiwe la Msingi la ujenzi wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi leo 5-1-2025, linalojengwa katika eneo la Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alipowasili katika viwanja vya Chuo Buyu kwa ajili ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 5-1-2025, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Prof.Bernadeta Killian akitowa maelezo ya kitaalamu ya ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linalojengwa katika eneo la Chuo Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe.Prof. Adolf Mkenda na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linalojengwa Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages