ALHAJJ HEMED AISHAURI JAMII KUUTUMIA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KULETA UMOJA KATIKA JAMII - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, March 8, 2025

ALHAJJ HEMED AISHAURI JAMII KUUTUMIA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KULETA UMOJA KATIKA JAMII

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na Viongozi na Wananchi mbali mbali katika Futari aliyoiandaa kwa ajili yao iliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Akitoa shukurani katika Iftari hiyo Alhajj Hemed amewashukuru Viongozi na Wananchi waliofika katika Iftari hiyo na kueleza kuwa mkusanyiko huo unaleta umoja katika jamii.

Aidha amewakumbusha waumini wa dini ya kiislamu kuendeleza tabia ya kuhurumiana na kusaidiana kwa kutoa walivyonavyo kwa makundi maalum ikiwemo Mayatima, Wazee, Wajane na Watu wenye Ulemavu hasa katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Amewasisitiza wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu kabla, wakati na baada ya uchaguzi ili kutoa fursa kwa serikali kuijenga zanzibar kimaendeleo.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Idriss Kitwana Mustafa amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuendeleza Ibada hiyo ya kufuturisha ikiwa ni kawaida kwa Viongozi na Waumini kufuturishana ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages