NBC Kutumia Mchezo wa Gofu Kuchochea Ushirikiano wa Kibiashara - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, March 24, 2025

demo-image

NBC Kutumia Mchezo wa Gofu Kuchochea Ushirikiano wa Kibiashara

1
Mkuu wa majeshi Mstaafu na Muasisi wa mashindano ya Gofu ya NBC Waitara Trophy, Jenerali George Waitara (katikati) akikabidhi zawadi ya kwa mshindi wa jumla wa mashindano ya NBC Waitara Trophy 2025 ‘Gofa’ mkongwe Edmund Mndolwa (wa tatu kushoto) kutoka klabu ya gofu ya Lugalo. Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa benki ya NBC. Wanaoshuhudia ni pamoja na Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Bi. Queen Siraki (kushoto), Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (wa pili kushoto), Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Muhimbili, Bw Aliko Mwamsaku (wa pili kulia) na Rais wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Gilman Kasiga.

Mashindano ya Gofu ya 'NBC Waitara Trophy 2025' yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa huku mdhamini mkuu wa mashindano hayo, benki ya NBC ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na wadau wa mchezo huo ili kuchochea ushirikiano wa kibiashara miongoni mwa wadau, kukuza na kuendeleza vipaji na kutangaza utalii.

Mashindano hayo yaliyofanyika kwa siku moja yakilenga kumuenzi muasisi wake Mkuu wa majeshi Mstaafu, Jenerali George Waitara yaliyohitimishwa na muasisi huyo kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki yakihusisha washiriki kutoka ndani ya nchi. Wachezaji walionyesha ujuzi, mbinu, na michezo ya kiungwana huku ‘Gofa’ mkongwe Edmund Mndolwa akiibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali wa mashindano hayo, Jenerali Waitara pamoja na kuwapongeza washiriki na wadhamini wa mashindano hayo, aliendeleza wito wake kwa jamii kushiriki kwa wingi kwenye mchezo huo bila kujali dhana ya kuwa mchezo hu oni mahususi kwa watu wa daraja la juu kiuchumi.

“Zaidi niendelee kutoa wito kwa kwa wadhamini wa mashindano mbalimbali ya mchezo huu yakiwemo mashindano haya kuangalia namna ya kupanua udhamini wao mbali na mashindano pekee pia waone namna ya kuboresha viwanja vya mchezo huu hususani kwenye mfumo wa umwagiliaji ili viweze kuwa katika hali nzuri hata kwenye msimu wa ukame.’’ Alisisitiza.

Akizungumza kwenye hafla hiyo muwakilishi wa benki ya NBC, Bw Aliko Mwamsaku, Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Muhimbili alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye mashindano hayo kwa kiasi kikubwa unasukumwa na adhma ya benki hiyo katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini ili kuibua vipaji, kuchochea ajira kupitia michezo pamoja na kuitumia vema sekta hiyo katika kutangaza utalii wa ndani.

“Pia kwetu mchezo wa gofu tunautazama kama moja ya michezo ya kimkakati inayoweza kuwasaidia wateja wetu kupata wasaa wa kujenga mahusiano ya ukaribu zaidi kupitia michezo na hatimaye mahusiano hayo yakaendelea hadi kwenye biashara zao binafsi na pia zile za taasisi zao kwa kuwa mchezo huu unatoa fursa kwa makundi tofauti ya wana jamii kuweza kukutana bila kujali umri, jinsia au daraja lolote kiuchumi.’’ Alisema Mwamsaku.

Akizungumzia ushindi wake Bw Mndolwa pamoja na kuwashukuru wadhamini wa mashindano hayo benki ya NBC, aliwapongeza wachezaji wenzake kwa ushindani mkubwa waliouonesha. Zaidi, Bw Mndolwa aliunga mkono wito wa Muasisi wa mashindano hayo Jenerali Waitara kuhusu uwepo wa mkakati wa makusudi kuhusu uboreshwaji wa uwanja huo hususani kupitia mfumo wa umwagiliaji.
2
Mkuu wa majeshi Mstaafu na Muasisi wa mashindano ya Gofu ya NBC Waitara Trophy, Jenerali George Waitara (katikati) akikabidhi zawadi ya kwa mmoja wa washindi kwa upande wa wanawake kwenye mashindano ya NBC Waitara Trophy 2025. Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa benki ya NBC. Wanaoshuhudia ni pamoja na Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Bi. Queen Siraki (kushoto), Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (wa pili kushoto), Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Muhimbili, Bw Aliko Mwamsaku (wa pili kulia) na Rais wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Gilman Kasiga.
3
Mkuu wa majeshi Mstaafu na Muasisi wa mashindano ya Gofu ya NBC Waitara Trophy, Jenerali George Waitara akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya NBC Waitara Trophy 2025. Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa benki ya NBC.
4
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Muhimbili, Bw Aliko Mwamsaku akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya NBC Waitara Trophy 2025. Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa benki ya NBC.
5
Mkuu wa majeshi Mstaafu na Muasisi wa mashindano ya Gofu ya NBC Waitara Trophy, Jenerali George Waitara (katikati - walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi mbalimbali wa mashindano ya NBC Waitara Trophy 2025. Mashindano hayo ya siku moja yalifanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu vya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa benki ya NBC.
6
7
Wadau wa mbalimbali wa mchezo wa Gofu wakiwemo viongozi wa mchezo huo wakifuatilia hafla hiyo.
8

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *