KAMPENI YA 'NO REFORM NO ELECTION' YAPOTEZA MWELEKEO RUKWA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, March 24, 2025

demo-image

KAMPENI YA 'NO REFORM NO ELECTION' YAPOTEZA MWELEKEO RUKWA

.com/blogger_img_proxy/
Mkutano wa kampeni ya No Reform No Election unaoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umeonyesha dalili za kupoteza mvuto baada ya kuwavutia idadi ndogo ya wananchi mkoani Rukwa, hususan katika Jimbo la Nkasi Kaskazini.

Tukio hilo lilitokea leo wakati viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Tundu Lissu, walipofika katika eneo hilo kuendelea na kampeni yao. Hata hivyo, mkutano huo uligeuka kuwa kichekesho baada ya waandaaji kugundua kuwa waliojitokeza kwa wingi ni watoto wadogo badala ya wapiga kura wenye sifa. Kutokana na hali hiyo, viongozi wa Chadema walilazimika kuwaimbisha nyimbo za watoto, jambo lililozua mijadala mbalimbali kuhusu mwelekeo wa kampeni hiyo.

Wachambuzi wa siasa wameeleza kuwa hali hii ni ishara kwamba ujumbe wa kampeni ya No Reform No Election haujapata uungwaji mkono unaotarajiwa na chama hicho, hasa katika maeneo ya vijijini ambako chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaendelea kushika hatamu. Pia, imezua maswali kuhusu mbinu za Chadema katika kuhamasisha wananchi kushiriki mijadala ya kisiasa na kudai mabadiliko wanayoyapigania.

Hali kama hii imekuwa ikijirudia katika mikutano kadhaa ya Chadema, ambapo idadi ya washiriki imekuwa ndogo na mara nyingine mikutano hiyo kuonekana kutowavutia wananchi wa kawaida. Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa hili linatokana na kutokuwa na ajenda inayowagusa moja kwa moja wananchi wa kawaida, huku wengine wakidai kuwa upinzani bado haujaweza kutoa mbadala wa sera unaoeleweka.

Huku CCM ikiendelea kutekeleza Ilani yake kwa vitendo, hali ya Chadema katika kampeni ya No Reform No Election inazidi kuzua maswali kuhusu nafasi yao katika siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi ujao. Ikiwa hali hii itaendelea, kuna uwezekano mkubwa kampeni hiyo ikapoteza mwelekeo zaidi, na hatimaye kufifia kabisa kabla ya kufikia malengo yake.
.com/blogger_img_proxy/
.com/blogger_img_proxy/
.com/blogger_img_proxy/

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *