TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI KUFANYIKA MIKOA YOTE TANZANIA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, March 24, 2025

demo-image

TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI KUFANYIKA MIKOA YOTE TANZANIA

Screenshot_20250324-153619_2
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Kamati ya maandalizi ya tamasha la Kuombea uchaguzi Mkuu  maalum linalotarajia kufanyika mikoa 26 ya Tanzania, likianza jijini Dar es Salaam yanaendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Machi 24, 2025, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema kuwa ibada hiyo itakuwa ni ya Maandalizi ya kuelekea Uchaguzi.

"Lengo ni kuweka umoja na ushirikiano watanzania kuombea uchaguzi kufanyika kwa Amani na kupata viongozi ambao watatuongoza kwa hekima na busara."

"Waimbaji kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda wanatarajia kupamba tamasha hilo la uimbaji na Maombi ya uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania."

Aidha ameongeza kwa kuwaomba viongozi wa vyama vya siasa kutumia lugha zisizo za matusi katika mikutano yao bali kutumia lugha za siasa zenye heshima hata kwa vizazi vyetu.

Pia amewaomba wadau na watu mbalimbali kujitokeza kutoa ushirikiano wa kudhamini ili kufanikisha tamasha hilo.

Alex Msama ni mwandaaji maarufu wa matamasha ya muziki wa injili nchini Tanzania kupitia kampuni yake, Msama Promotion. Amejulikana kwa kuandaa matamasha makubwa ya kiroho yenye lengo la kuombea nchi, viongozi, na jamii kwa ujumla.

Katika miaka ya nyuma, Msama ameandaa matamasha kama Tamasha la Pasaka na Tamasha la Krismasi, ambayo yamekuwa na mwitikio mkubwa, yakishirikisha waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania. Pia, amekuwa mstari wa mbele katika kutumia matamasha hayo kuhamasisha amani, mshikamano wa kitaifa, na maombi kwa ajili ya viongozi wa taifa.

Kwa tamasha la sasa la kuombea Uchaguzi Mkuu, inaonekana anaendeleza juhudi zake za kutumia muziki wa injili kama jukwaa la kuhamasisha maadili mema na utulivu wa nchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *