TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, March 8, 2025

TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA

 


Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuahirisha mechi ya ‘dabi’ ya Kariakoo ambayo ilipangwa ichezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, kuahirishwa kwa mechi hiyo kumekuja baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Kuu Tanzania, kupitia shauri la klabu ya Simba kuzuiliwa kuingia katika dimba la Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya leo kuvaana na wenyeji wao Yanga SC.

“Bodi ilipokea taarifa ya afisa usalama wa mchezo huo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyoambatana na tukio la Simba kushindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema, bodi imeahirisha mchezo huo ili kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kufanya maamuzi ya haki.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages