KATIBU MKUU VIWANDA ATEMBELEA BANDA LA FCC MAONESHO YA SABASABA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, July 1, 2025

KATIBU MKUU VIWANDA ATEMBELEA BANDA LA FCC MAONESHO YA SABASABA

Katibu Mkuu Viwanda na Biashara, Dkt. Ashil Abdallah ametembelea Banda la Tume ya Ushindani (FCC), katika ziara yake ya kukagua Banda Jumuishi la Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, yaliyoanza Juni 28, 2025 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika Banda la FCC, Dkt. Ashil amepongeza maandalizi yaliyofanywa na Taasisi hiyo, nakwamba ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara kutumia maonesho hayo kupata huduma katika Taasisi hiyo.

Aidha, ameonesha kuridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na Wizara hiyo, inayosimamia Taasisi 14 ambazo zinashiriki maonesho ya mwaka huu.

FCC ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara yenye jukumu la kulinda na kushajiisha ushindani, kumlinda mlaji na mtumiaji dhidi ya mienendo potofu, kandamizi na hadaifu katika uchumi wa soko na udhibiti wa bidhaa bandia nchini.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages