
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga kiwanda Cha kuchakata machungwa na matunda mengine.
Ametoa ahadi hiyo katika mkutano wa kampeni za CCM Mjini Muheza mkoani Tanga Septemba 29,2025.
Aidha, Dkt. Samia amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kuchaguliwa kwa kura nyingo Oktoba 29, 2025, atakikisha serikali inajenga barabara ya lami ya Pangani - Muheza yenye urefu wa Km 45 ambayo hata yeye amepita akitokea Pangani.


No comments:
Post a Comment