SERENE SAFARI BUREAU DE CHANGE YAZINDULIWA ARUSHA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, September 29, 2025

SERENE SAFARI BUREAU DE CHANGE YAZINDULIWA ARUSHA

Na Pamela Mollel, Arusha

Tanzania inaendelea kupiga hatua kubwa katika sekta ya fedha ambapo kijana mwekezaji wa kike, Mishel Mrema, amepongeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupigania ndoto za vijana wa Kitanzania na kutoa fursa za kufanya uwekezaji bila ubaguzi.

Alisema anamshukuru Rais Samia kwa kupambania vijana katika kipindi chake cha urais kwa kunyanyua vijana.

Mrema aliongeza kuwa Rais ameweza kuinua vijana kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo, utalii, uchumi na huduma za kifedha kama Bureau de Change. Pia alibainisha kuwa kupitia Royal Tour, wageni kutoka mataifa mbalimbali wamefanikisha fursa nyingi za huduma za kifedha nchini.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi pamoja na wageni kutembelea taasisi hiyo ili kubadilishana fedha jijini Arusha, akibainisha kuwa Serene Safari Bureau de Change inalenga kutoa huduma bora za ubadilishaji fedha za kigeni sambamba na kusaidia vijana kupata ajira.

VIONGOZI WAPONGEZA HATUA HIYO

Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi huo jijini Septemba 27,2025, Iris Naushad Makere, Kamishna wa Mkoa wa Tanzania Girl Guides, alisema kuwa maadili, bidii na roho ya kujituma vimekuwa dira ya maendeleo ya taasisi hiyo. Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa taasisi ya kifedha kama Serene Safari Bureau de Change ni ubunifu wenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa la Tanzania.

Kwa upande wake, Hashim Chamani, Mkurugenzi wa Furaha Safari Bureau de Change, alieleza furaha yake kwa ujio wa taasisi hiyo mpya akisisitiza kuwa itaongeza ushindani wa kibiashara, kuboresha huduma za kifedha na kuchangia ajira kwa vijana. Chamani pia alimpongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuwezesha makundi yote ya Watanzania, wakiwemo vijana.

ISHARA YA MWAMKO MPYA

Uzinduzi wa Serene Safari Bureau de Change unaashiria mwamko mpya wa wanawake na vijana katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia sekta ya kifedha. Ni ishara ya nafasi kubwa ya uwekezaji na mchango wa kizazi kipya cha Watanzania katika kujenga uchumi wa taifa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages