DKT. SAMIA ATOA ELIMU NAMNA YA KUPIGA KURA OKTOBA 29,2025 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, October 7, 2025

DKT. SAMIA ATOA ELIMU NAMNA YA KUPIGA KURA OKTOBA 29,2025

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha mfano wa karatasi ya kupigia kura kwa maelfu ya wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jijini Mwanza Mkoani Mwanza leo Jumanne Oktoba 07, 2025 kwenye Viwanja vya Nyamagana wakati wa Mkutano wake wa hadhara wa Kampeni.

Karatasi halisi yenye kufanana na mfano huo ndiyo itakayotumika siku ya upigaji kura siku ya Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ambapo juu kabisa ndipo lilipo jina la Chama Cha Mapinduzi, Jina la Mgombea wake Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi sambamba na picha zao ambapo alama yako ya tiki upande wa kulia mwa picha zao ndio uthibitisho wa kura yako katika kuwapa ridhaa ya kuunda serikali itakayoongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo.

Pembeni ya Dkt. Samia ni Katibu wa NEC, Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Kenani Laban Kihongosi. Mfano huo wa karatasi za kupigia kura imetolewa kwa Vyama vyote vya siasa ili kutumika kama sehemu ya kutoa elimu kwa wapiga kura ili kutokufanya makosa kwenye chumba cha upigaji wa kura.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages