
Dar es Salaam: Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, amesema kuwa sekta ya utalii imeendelea kuimarika kutokana na kuongezeka kwa weledi wa wadau mbalimbali vikiwemo vyuo vitavyowaanda vijana wenye uwezo wa kumudu soko la ajira, ndani na nje ya Tanzania.
Waziri Chana aliyasema hayo wakati alipozindua Warsha maalum iliyolenga kkuwajengea wezo wadau wa sekta hiyo, kuhusu usimamizi wa hoteli kwa mazingira rafiki, viwango vya uidhinishaji wa kijani kibichi, na mifumo bora ya udhibiti wa taka, iliyofanyika Oktoba 7, 2025 katika Chuo cha Taifa cha Utalii NCT, Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa mafanikio hayo yamechagizwa na uwepo wa Filamu ya Tanzania 'The Royal Tour' iliyoandaliwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ambayo imesababisha kuongezeka kwa watalii, na kuimarisha sekta nzima ya utalii nchini.
Aidha, waziri Chana, aliipongeza NCT kwa jitihada zake za kutoa mafunzo ya kitaalamu katika masuala ya Utalii na Ukarimu kwa vijana ambapo maarifa na ujuzi wanaopata kunawawezesha ushindana katika soko la ajira kimataifa.
Alisema Warsha hiyo inaakisi dhamira ya Tanzania katika kujenga mustakabali mzima kwenye masuala ya ukarimu unaoendana na uwajibikaji.
"Warsha hii inaakisi dhamira yetu ya kina ya kujenga mustakabali ambapo ubora katika ukarimu unaendana na uwajibikaji kwa mazingira na jamii zetu. Mafunzo yetu yamejikita katika maadili ya Kitanzania huku tukikumbatia viwango vya kimataifa" alisema Dkt. Chana.
Aidha alibainisha kuwa katika kipindi hiki cha ulimwengu uliojaa teknolojia suala la uendelevu si hiari tena, bali ni la umuhimu na lazima, nakwamba wadau wanapaswa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kimaadili na ubunifu ili kuhifadhi mazingira na tukikuza sekta nzima kwa ujumla.
Akizungumza alipokuwa akitoa mada katika warsha hiyo, mtaalam wa masuala ya utalii kutoka Chuo Kikuu cha RUDN, Urusi Prof. Denis Chistyakov, amesema ushirikiano wa kimataifa katika kujenga mustakabali endelevu.
"Ushirikiano wetu na NCT unawakilisha daraja kati ya mabara - kuleta utafiti, maarifa na uvumbuzi kwa muktadha wa ndani ambao ni muhimu sana."
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha NCT Dkt. Florian Mtey, amesema kuwa Chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali katika myooro mzima wa sekta ya utalii, nakuchagiza uwepo wa wadau wenye weledi wanaokidhi vigevyo vya Kitaifa na Kmataifa katika soko la Ajira.
Aidha amekipongeza Chuo Kikuu cha RUDN cha Urusi kwa mashirikiano yao yenye kuleta faida kubwa kwa wakufunzi na wanafunzi wa Taasisi yao.





No comments:
Post a Comment