Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Modest J. Mero akitoa maelezo mafupi kwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe.
António Guterres kabla ya kuwasilisha rasmi Hati za Utambulisho.
Balozi. Modest J. Mero akiwasilisha Hati za Utambulisho
kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe.
António Guterres.
Balozi. Modest J. Mero na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe.
António Guterres wakipeana mikono baada ya zoezi la kuwasilisha Hati za
Utambulisho kukamilika.
Balozi. Modest J. Mero na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe.
António Guterres wakisalimiana na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja
wa Mataifa waliokuwepo kushuhudia tukio la kukabidhi Hati za Utambulisho (pichani
wakisalimiana na Bw. Songelael Shilla, Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania
kwenye Umoja wa Mataifa, New York).
Akizungumza baada ya makabidhiano ya Hati
za Utambulisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres alisema Umoja wa
Mataifa unaishukuru Tanzania kwa jinsi inavyojitolea kwa hali na mali katika
jitihada za kumaliza migogoro ya kisiasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Alitaja hatua zinazochukuliwa na Tanzania kurejesha amani DRC, Burundi na Sudan Kusini kuwa ni mfano wa kuigwa na kwamba anayo imani kwamba jitihada hizo hazitakoma mpaka nchi za SADC na EAC zote ziwe na utulivu wa kisiasa.Naye Balozi Mero akitoa neno la shukurani, alimuahidi Bw. Guterres ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kufanikisha malengo ya maendeleo na ulinzi wa amani.

Aidha, alimwonyesha matarajio iliyonayo Tanzania kwake kwa kuzingatia
ushirikiano mzuri aliounesha wakati alipokuwa akishughulikia masuala ya
wakimbizi duniani, ambapo kwa pamoja na serikali ya Tanzania waliweza
kutekeleza mengi kwa mafanikio makubwa
No comments:
Post a Comment