Serikali ya Korea kupitia mradi wa ''Thank you Small Library program''
leo imekabidhi Vifaa na kuzindua maktaba ndogo ya kisasa katika ofisi za
makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo balozi wa
Korea nchini Song Geum Young amesema kuwa serikali yake licha ya kusaidia
serikali katika miradi mingi lakini kwa sasa wameamua kusaidia katika
kuwawezesha watoto kupata elimu inayoendana na wakati.
"Sisi kama Korea tunaamini kuwa ukimpa mtoto elimu umeweza kumpa
maisha ya kesho, hivyo vifaa hivi vitaweza kuwasaidia katika kukuza taaluma yao
" amesema Balozi.Balozi ametoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto waweze
kutumia maktaba hiyo kwa kutumia sehemu hiyo kwa ajili kukuza taaluma yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard
Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young na Mama Anna Abdalah
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa wakikata
utepekuashiria uzinduzi huo.
Balozi
wa Korea nchini, Song Geum Young akizungumza kabla ya uzinduzi wa wa Maktaba ya
kisasa ambayo imetolewa na Serikali ya korea.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo, akikabidhi vitabu kwa
Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa, Mama Anna Abdalah.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa, Audax Mabula akizungumza kabla ya uzinduzi wa
Maktaba ya Kisasa katika Makumbusho ya Taifa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akizungumza kabla ya uzinduzi
wa Maktaba ya Kisasa katika ukumbi wa Makumbusho ya taiafa kwa msaada wa
Serikali ya watu wa Korea.
Baadhi
ya wadau walioshiriki tukio hilo
Viongozi mbalimbali akiwemo
na balozi mteule wa korea wakifatia hotuba ya balozi
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Bunge wakishuhudia tukio hilo
Mwenyekiti
wa bodi ya Makumbusho ya Taifa, Mama Anna Abdalah akizungumza na waandishi wa
habari
Wanafunzi wa
shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika Maktaba ya
Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika Maktaba ya
Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na Balozi wa Korea nchini,
Song Geum Young wakipata maelekezo jinsi ya namna vifaa vya kielektronic
vinavyofanya kazi katikakutoa elimu kwa watoto ndani ya maktaba hiyo ambayo
imefadhiliwa na serikali ya Korea
Picha
ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na
Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young na Mama Anna Abdalah wageni waalikwa
wengine waliohudhuria katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment