Ubalozi
wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam jana.
Shule za
Msingi zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja , Mwale pamoja na Bwawani.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem amesema
kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndio maana wameona umuhimu wa visima hivyo
katika shule hizo.
Amesema
wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika jamii
kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.
Al-Najem
amesema kuwa wamefanikiwa kuchimba visima 16 vyenye thamani ya Dola za
Kimarekani 63,000 na watu wengine wanaweza kujitokeza kusaidia jitihada
mbalimbali.
Ubalozi
huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani
sh.milioni tatu.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji
katika shule ya Yombo iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam jana,
Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene, Anwari Abdallah Al-Hasawi.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem kushoto na Naibu Mkurugenzi wa
Red Cresene, Anwari Abdallah Al-Hasawi wakinywa maji mara baada kuzindua kisima
katika shule ya msingi Yombo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala, Hamisi Mlangala
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada huo
jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu
Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto
katika Hospitali ya Amana jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akimsikiliza Mganga Mkuu
Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment