Bocco ‘fiti’ kuivaa Stand, Azam ikijiandaa dhidi ya Mbabane Swallows - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, March 3, 2017

Bocco ‘fiti’ kuivaa Stand, Azam ikijiandaa dhidi ya Mbabane Swallows

MAKAMU bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara na FA Cup, timu ya Azam FC inataraji kumkaribisha tena kikosini nahodha na mshambuaji wao namba moja John Bocco katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Stand United siku ya kesho Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi.
Azam FC ambayo iliifunga Mtibwa Sugar na kutinga robo fainali katika michuano ya FA inataraji kuutumia mchezo huo dhidi ya Stand kama maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Caf Confederation Cup dhidi ya Mbabane Swallows FC mwishoni mwa wiki ijayo.
“Tunamshukuru Mungu maandalizi yetu yanaendelea vizuri, kasoro pekee ni kwamba tutaendelea kukosa huduma ya kiungo wetu raia wa Cameroon, Stephan Kingue  ambaye alipata majeraha katika mchezo wetu dhidi ya Simba mwezi uliopita, lakini habari nzuri ni kwamba John Bocco amerejea na atakuwepo kwenye mchezo wa kesho panapo majaliwa kama mwalimu ataamua kumtumia. Kiujumla maandalizi yako sawa hadi sasa,” anasema meneja wa Azam FC, Phillip Alando.
“Kocha anauchukulia kwa umuhimu mkubwa mchezo huo ukizingatia kwamba tulimfikishia taarifa za kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza kule Shinyanga dhidi ya hawa Stand kwa hiyo mwalimu anaiona kama timu ambayo inapigana hivyo hana mzaha kabisa katika maandalizi yake kuelekea mchezo huo.”
Azam FC ilifungwa 1-0 katika uwanja wa Kambarage katika mchezo ambao mlinzi wa timu hiyo Aggrey Morris alimchezea vibaya mshambulizi wa Stand, Chidiebele Abasarim kiasi cha kupelekea Mnigeria huyo kuvunjika taya.
“Kocha anahitaji pointi tatu ili kufanya timu iwe katika nafasi nzuri zaidi kwenye ligi. Nachoweza kuwaambia mashabiki wa Azam kwamba, tutajitahidi kuchezavizuri ili kupata ushindi na niwaombe waje kwa wingi ukizingatia kwamba mechi yetu ya kesho itakuwa ya mwisho kabla hatujacheza mchezo wetu dhidi ya Mbabane Swallows kwenye michuano ya Confederation, hivyo waje kutazama nini ambacho mwalimu amekiandaa kuelekea mchezo wa Caf.”

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages