Kampuni
ya Bonite Bottlers Kupitia kinywaji chake cha Coca-Cola imezidi kuhamsisha
wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao kupitia Promotioni ya Onja Msisimko na
Coca-Cola wanayoiendesha katika shule mbalimbali jijini Arusha. Cocacola
imefanya hayo katika shule Sekondari ya Olorieni jijini Arusha ambapo baadhi ya
wanafunzi walipata Fursa ya kuonyesha vipaji vyao ikiwemo kucheza na baiskeli
katika jukwaa, kucheza muziki pamoja na kuimba. Msimamizi wa promosheni hiyo
Onesmo Swila amewataka wanafunzi katika shule hizo wanazotembelea ikiwemo
Sekondari ya Olorieni ambayo wameitembelea, kuendeleza vipaji vyao kwa kila
fursa wanayopata kwa kuwa kipaji ni hazina.
“wanafunzi
acheni kuficha vipaji vyenu, vionyesheni, ili mpate fursa ya kuvikuza, sisi
Coca-Cola tumeamua kuwahamasisha kwa lengo kuwatia moyo ili mfikie malengo
yenu.” Alisema Onesmo Aidha licha ya kuwashukuru walimu wa shule hiyo kwa
kuwakubalia kutembelea shule hiyo na kuwagawia wanafunzi zawadi ikiwemo ya
kinywaji cha Coca-Cola, amesema ziara hiyo wataendelea nayo katika shule
mbalimbali jiji Arusha ili kuwaonjesha wanafunzi Msisimko wa Coca-Cola.
Mwalimu
wa Michezo katika Shule ya Sekondari ya Olorieni, Haroon Maluli akipokea zawadi
ya Mipira kutoka Coca-Cola, Ameshukuru kwa zawadi hiyo huku akiwasihi wanafunzi
kutoficha vipaji vyao, bali wavionyeshe kwa kila fursa inayopatikana ili
kuvikuza zaidi. “Tunashukuru kwa zawadi ya mipira, ila nawasihi wanafunzi
kutumia fursa kama hii iliyoletwa na Coca-Cola kuonyesha vipawa vyenu, kwani
hata sisi tulivyokuwa tunasoma hatukuvificha ndio maana tupo hapa” alisema
Mwalimu Haroon.
Wafanyakazi wa Coca-Cola wakiwagawia wanafunzia wa Shule ya Sekondari
ya Olorieni Vinywaji vya Coca-Cola katika eneo la shule hiyo.
Mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni akionyesha kipaji cha
kucheza na Baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja
msisimko katika shule mbalimbali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha
kucheza na baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja
msisimko katika shule mbalimbali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso
(jukwaani) huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na
Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
Wanafunzi wa wawili wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha
kipaji cha kucheza muziki kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola katika
shule mbalimbali.
Mwongozaji wa Promosheni (Supervisor) Onesmo Swila Akimkabidhi zawadi
ya mipira ya miguu mwalimu wa michezo wa shule ya Sekondari ya Olorieni katika
promosheni yao ya Onja msisimko na Coca-ola inayoendeshwa katika shule
mbalimbali jijjini Arusha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha
kuimba kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika
shule mbalimbali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso
(jukwaani) huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola
ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakigongeana sheazi mara
baada ya kugawiwa vinywaji kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja
msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment