Mwanamitindo maharufu nchini, Jokate Mwegelo
amewataka watoto kike kujiamini hili waweze kufikia mafanikio katika maisha
hayo kwa kuweka juhudi katika elimu.
Jokate amesema hayo leo katika mahadhimisho ya siku
ya Wanawake Duniani alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kike katika shule ya
sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam.
“nataka niwaambie watoto wa Manzese sekondari siri
kubwa ya mafanikio ni kujiamini lakini usijiamini katika ujinga hivyo mnapaswa
kujiamini katika vitu vya msingi ambavyo viatweza kusaidia jamii yetu kutoka
sehemu moja kwenda nyingine” amesema Jokate.
Kwa upande wake program meneja wa TAI, Edith James amesema
kuwa umefika wakati wa wanawake kujiamini hasa kwa kupata elimu bora juu ya
afya ya uzazi na usafi wa mwili kwa ujumla hasa wakati wanapokuwa katika siku
zao.
Amesema kuwa taasisi ya TAI imekuwa katika kampeni
kwa zaidi ya shule kumi za mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa elimu kwa watoto wa
kike waweze kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi.
Jokate Mwegelo akipima
afya katika zoezi liliondeshwa shule ya sekondari Manzese jijini Dar es Salaam.
Mwanamitindo Jokate
Mwegelo akizungumza na Mabinti wa shule ya Sekondari Manzese jijini Dar es
Salaam juu ya kujitambua na kujiamini hili kufikia mafanikio
waliyojiwekea.
Mratibu kutoka taasisi
isiyo ya kiserikali ya TAI, Edith James akizungumza na mabinti wa shule ya
sekondari Manzese.
Picha kwa juu ikionyesha
namna Jokate alivyokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese.
Jokate akiwa katika picha
ya Pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese
Daktari kutoka tasisi ya
TAHMEF, Victoria Joseph akitoa maelekezo juu ya tasisi yao inavyotoa
huduma kwa watoto wa kike mashuleni
Joakate Mwegelo
akikabidhi taulo za kike kwa mmoja wanafunzi wa sekondari ya Manzese jijini Dar
es Salaam
Mkurugenzi wa kampuni ya
Kays Hygiene product Malik Mtui akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari
Manzese
No comments:
Post a Comment