Mhe.
Kairuki akimsikiliza mmoja wa watumishi wa Sekretarieti ya maadili ya
viongozi wa umma kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya alipowapa
fursa watumishi hao kutoa maelezo ya vikwazo wanavyopambana navyo .
Katibu
wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Erick Mbembati
(aliyevaa suti nyeusi) akimwonyesha Mhe. Angellah Kairuki kiwanja
kinachotarajiwa kujengwa Ofisi za sekretarieti hiyo jijini Mbeya.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
mhe. Angellah Kairuki akifungua bomba la maji lililojengwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii- TASAF – katika kijiji cha Majengo katika wilaya ya
Mbarali mkoani Mbeya, wa kwanza kushoto ni mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,
Ladislaus Mwamanga.
Waziri
Kairuki akimwangalia Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga
anayekunywa maji kutoka kisima kilichochimbwa na TASAF katika eneo la
Majengo, Wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.
Waziri Angellah
Kairuki akikagua kwa dhati moja ya kitambusho cha mlengwa wa Mpango wa
kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na TASAF katika kijiji cha Majengo, wilaya Mbarali mkoani Mbeya wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani
hu. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga.
Hapa
ni furaha kubwa,Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa
umma na utawala bora, Angellah Kairuki akiwa ameketi katika nyumba
iliyojengwa na mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Majengo,
Gervas Ngei (mwenye shati ya drafti) kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga aliyevaa miwani.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa
wa TASAF Bw. Gervas nje ya nyumba aliyoijenga kwa kutumia fedha za
ruzuku zinazotolewa na Mfuko huo kwa takribani kaya milioni MOJA NA LAKI
MOJA nchini kote. Mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,
Ladislaus Mwamanga.
Waziri
Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa
TASAF na halmashauri ya wilaya ya Mbarali nje ya nyumba iliyojengwa na
mmoja wa walengwa wa Mfuko huo katika kijiji cha Majengo , Gervas
Ngei kwa kutumia fedha alizozipata baada ya kulima mpunga kwa ruzuku
hiyo.
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora,
Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa
Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Nyanda za juu
kusini jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment