Msanii wa muziki wa Hip pop Kala Jemiah amedai kuwa
amefanya tafiti ndogo juu ya muziki wa sasa na mashabiki wake na kugundua
kuwa kiki ni kitu muhimu sana katika muziki wa sasa ili kukuza jina na muziki
unaofanya, bila kutafuta kiki au kufanya kitu ambacho mashabiki wako
watakuongelea muda wote inapelekea kusahaulika kimuziki.
Kala Jeremiah alizungumza kwa upande wake hawezi kutafuta
kiki kwani anaamini ameshazeeka, majukumu ya kifamilia yameongezeka na kuna baadhi
ya vitu ambavyo amezungumza kuaachana navyo kwani tayari ana mtoto.
Hali hii ni tofauti na muziki wa zamani, miaka ile msanii
alikuwa anajulikana kupitia muziki wake au albamu yake aliyoifanya.
”Muziki wa sasa umebadilika kutokana na mashabiki kutaka vitu
fulani ambavyo sio vya kawaida,” amesema Kala Jeremiah.
Katika tafiti ndogo aliyoifanya amegundua jina la rapa,
Harmorapa ni kubwa kuliko hata majina ya baadhi ya wasanii wa muziki huo ambao
tayari wana albamu mbili sokoni.
”Mimi hivi karibuni nilikuwa na msichana mmoja nikataka
kujua nguvu za baadhi ya wasanii wa hip pop, nikawa namuuliza kuhusu wasanii
watano ambao wengine wana albamu zaidi ya mbili sokoni alisema hawajui, lakini
nilipomuuliza kuhusu kumjua Harmorapa alijibu kuwa huyo namjua sana, tena ana
wimbo mmoja,” amesema Kala Jeremiah.
Ameongeza kwa kusema, ”kwaiyo nikagundua huu mziki sasa
hivi msanii anatakiwa kuzungumziwa kila mara, sio ukitoa tu ngoma basi, kuna
namna ambavyo unaweza kufanya ili uendelee kuwa midomoni kwa mashabiki”.
Ukifanya tafakari ndogo juu ya tafiti na mtazamo wa mwana
Hip pop Kala Jeremiah, utagundua kuna ukweli ndani yake siku hizi watu
wanatafuta njia ya kutokea kimuziki kwa kutafuta visa ili wajadiliwe mitandaoni
na katika vyombo vya habari.
Ni jambo zuri na jema kutengeneza jina mtaani kwanza
kisha kuzama katika mziki maana tayari utakuwa unajulikana kwa kitu
fulani ambapo ukiingia kwenye muziki ni rahisi watu kutaka kuujua muziki wako
zaidi kama ilivyo kwa Harmorapa, Luludiva na Mimi Mars, ambao ni chipukizi
lakini muziki wao unafanya vizuri sokoni.
No comments:
Post a Comment