Tundu Lissu,
Mwanasheria Mkuu wa Chadema (katikati) akizungumza na vyombo vya habari muda
mchache baada ya kutoka kuhojiwa na polisi
HATIMAYE Tundu Lissu, Mbunge wa
Jimbo la Singida Mashariki, ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam baada ya kufutiwa mshitaka na kukamatwa tena jana
asubuhi kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kidini.
Lissu alikamatwa akiwa ndani ya Mahakama ya Kisutu baada ya
serikali kuwasilisha taarifa kuwa haina nia ya kuendelea na kesi iliyofungua
hapo awali na kisha polisi kumpeleka kituo ch kati kwa mahojiano.
Taarifa
zilizopatikana jana jioni zinaeleza kuwa Lissu amehojiwa juu ya kauli yake
aliyoitoa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar miezi miwili
iliyopita pale alipotamka kuwa “Uchaguzi w Zanzibar ulikuwa haramu kama muislam
kula nyama ya nguruwe.”
Hata
hivyo inadaiwa kuwa Lissu ameachiwa lakini simu zake za mkononi zimeendelea
kushikiliwa na polisi na kwamba atatakiwa kuripoti tena manmo tarehe 13 Machi
mwaka huu katika kituo cha polisi cha kati.
Mapema jana
asubuhi baada ya kukamatwa Lissu alindika ujumbe ukisema, anaamini kukamatwa
kwake kuna uhusiano wa moja kwa moja uchaguzi ujao wa Chama cha Mawakili hapa
nchini (TLS), unaotarajia kufanyika wiki mbili zijazo.
“Serikali hii, kwa kutumia mawakili wao vibaraka, imekuwa na
mkakati mkubwa wa kunizuia kugombea urais wa TLS. Walipanga kwenda kupinga kugombea
kwangu mahakamani. Tumewasema hadharani na kuzianika njama zao. Sasa wameamua
kutumia rungu lao la siku zote,” alisema.
No comments:
Post a Comment