RAIS Dk.
John Magufuli ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu
wa Shirika Elimu Kibaha Dkt. Crspin Mpemba ili kupisha
uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema kufuatia
tuhuma mbalimbali za uendeshaji, zinazolikabili Shirika hilo ambazo zimekuwa
zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.
Simbachawene
amesema Mnamo Machi, 4 mwaka huu Rais Magufuli ametengua rasmi nafasi ya
Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Amefafanua
kuwa kumekuwepo malalamiko dhidi ya Mtendaji Mkuu wa wa
shirika la Elimu Kibaha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI iliunda kikosi
kazi ili kufanya uchunguzi dhidi ya malalamiko hayo na kugundua
kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji wa Shirika hilo.
“Ni kweli
tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba
iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara
hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili
kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja
zinazohitaji uchunguzi zaidi,” ameeleza Waziri Simbachawene.
Ameongeza
kuwa ili uchunguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru Mhe. Rais ameamua kumsimamisha
kazi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina
dhidi yake.
No comments:
Post a Comment