Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha kuwa linaboresha mawasiliano yake
baina ya wananchi wanaoishi maeneo jirani na hifadhi wameamua kuwapa mafunzo
maalum ya wiki moja yanayolenga kuwajengea uwezo Wahifadhi Ujirani Mwema katika
kutekeleza majukumu yao ya kila siku hususan utoaji wa Elimu ya Uhifadhi kwa
wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi nchini.Miongoni mwa mammbo
ambayo wameweza kujifunza ni utoaji taarifa kwa njia ya habari. Ilikufanikisha
hilo TANAPA imewapa mafunzo ya kitaalam maofisa wake hao katika mafunzo
yanayoendelea mjini Dodoma. Pichani juu ni Mhariri wa Habari Mwandamizi wa
Machapisho ya Mwisho wa wiki ya Gazeti la Habarileo, kutoka Kampuni ya Magazeti
ya Serikali (TSN), Oscar Mbuza akitoa mafunzo ya uandishi bora wa habari za
kijamii kwa maofisa hao.
Maofisa Uhifadhi Ujirani
mwema kutoka hifadhi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo ya
uandishi wa habari.
Maranyingi habari
huendana na picha, ili somo hilo la Habari liwezuri na liende sawa maofisa hao
pia walipewa mafunzo ya namna ya upigaji picha bora za Habari na namna ya
kutumia Kamera. Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Mroki
Mroki alitoa mafunzo hayo kikamilifu.
Muda wa majadiliano
ulikuwepo baada ya kutoa mada, ambapo pia maswali yaliulizwa na kujibiwa.
Washiriki wakifuatilia
kwa umakini somo la upigaji picha.
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi nae alishiriki mafunzo hayo
kama mwenyekiti wa mafunzo.
Washiriki wakiendelea na
mafunzo.
No comments:
Post a Comment