Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Obadia Kameya akifungua semina ya elimu ya sheria za kodi iliyofanyika
katika ukumbi wa Benki Kuu ambapo washauri wa masuala ya kodi walijadili namna
ya utekelezaji wa mabadiliko mbalimbali katika sheria za kodi nchini.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza wakati wa semina ya kujadili
namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko katika sheria za kodi iliyofanyika
katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Washauri wa masuala ya Kodi (Tax Consultants) walioshiriki katika
semina ya kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko ya sheria za kodi
nchini iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na
kampuni ya ushauri wa masuala ya kodi ya Hanif Habib & Co.Semina hiyo
ilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu jijini dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Obadia
Kameya akiwa katika picha ya pamoja na Washauri wa masuala ya kodi (Tax
Consultants) baada ya semina ya majadiliano ya namna bora ya utekelezaji wa
mabadiliko na maboresho katika sheria za kodi nchini kuisha.Semina hiyo
ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment