Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa
Benki ya Exim, Seleman Ponda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kushoto ni Mkuu wa kitengo cha fedha
msaidizi wa Benki hiyo Issa Hamisi na
mwengine ni Meneja Mkuu fedha Joseph
Mrawa
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Ponda akisisitiza jambo kuhusu na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Masoko wa Benki ya Exim Abdulrahman
Nkondo (aliyesimama), akitoa utambulisho kwa waandishi wa habari viongozi wa Benki hiyo waliohudhuria hafla hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Msaidizi wa
Benki ya Exim, Issa Hamisi akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo
katika ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya
Exim, Seleman Ponda akitoa maelezo ya kina kwa waandishi wa habari kuhusu na Matokeo ya
Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam jana kushoto ni Mkuu wa kitengo cha fedha msaidizi wa Benki hiyo
Issa Hamisi.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Msaidizi wa
Benki ya Exim, Issa Hamisi Seleman Ponda
akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu Matokeo ya Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika
ghafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya
Exim, Seleman Ponda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya
Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam jana kulia ni Meneja
Masoko wa Benki ya Exim Abdulrahman Nkondo katikati ni Mkuu wa kitengo cha
fedha msaidizi wa Benki hiyo Issa Hamisi.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Msaidizi wa
Benki ya Exim, Issa Hamisi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya
Exim, Seleman Ponda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu na Matokeo ya
Mahesabu ya fedha mwaka 2016 kwa benki hiyo katika ghafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam jana kulia kwake ni Meneja Mkuu fedha wa Benki hiyo Joseph Mrawa.
Aprili 3 2017, Dar es Salaam
Benki ya
Exim imepata faida ya Tsh bilioni 83.6 (kabla ya kodi) kwa mwaka wa fedha 2016 ikiwa
imejumuisha faida ya Tsh bilioni 46.4 ya kuuza hisa ilizowekeza. Faida
itokanayo na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibenki ni Tsh 37.2 Bilioni.
Mapato yatokanayo
na riba yaliongezeka kwa asilimia 25 mpaka Tsh 90.9 bilioni, ikiwa imechangiwa
na ongezeko la mikopo pamoja na mkazo katika amana zenye riba nafuu.
Aidha
katika kipindi hicho hicho, mapato yatokanayo na tozo mbalimbali za huduma za
kibenki yaliongezeka kwa asilimia 14 mpaka Tsh bilioni 35.7 ukilinganisha na
Tsh bilioni 31.3 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa
na ufanisi kwenye utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.
Faida hiyo
imeongeza mtaji wa benki kufika Tsh bilioni 227 na kuongeza uwezo wa benki
kuweza kufanya miamala ya kibiashara mikubwa zaidi.
Katika
kuongeza uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kujiandaa kwa ukuaji wa
kasi, Benki ya Exim imetelekeza miradi mbalimbali ya kiteknolojia.
“Nina
furaha kubwa kuwataarifu kwamba kati ya miradi 8 ya kiteknolojia, miradi 7
imemalizika kwa mafanikio”. Alisema Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo
Bw. Selemani Ponda na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia, benki
itaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.
Utekelezaji
wa miradi hiyo kwaajili ya kubadilisha mifumo ya kiutendaji umepelekea
uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu na teknolojia na hivyo kusababisha
gharama za uendeshaji kupanda. Katika taarifa yake ya fedha jumla ya gharama ya
uendeshaji ilipanda kwa asilimia 24 hadi
kufikia Tsh bilioni 99.
Benki ya
Exim imejiandaa kuwahudumia wateja wa kada zote kutokana na kuongezeka kwa uwezo
wa kuhudumia wateja wote mara baada ya kutekeleza miradi ya kiteknolojia na
kuongezeka kwa mtaji.
Akizungumzia mafanikio ya benki tanzu za Exim
zilizopo katika nchi tatu: Komoro, Djibuti na Uganda, Bw. Ponda alisema kuwa
Komoro na Djibuti wamefanya vizuri na kuweza kupata faida mara 3 ya mwaka
uliopita na kufikia Tsh bilioni 8 kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi na huduma
bora. Na benki tanzu mpya ya Uganda ilipata hasara ndogo ya Tsh milioni 177, na
inategemewa kufanya vizuri zaidi mwaka huu baada ya kuteleza mikakati mipya
baada ya Benki ya Exim kununua hisa zaidi ya 58.6%.
No comments:
Post a Comment