Tanga Cement yazidi kujitolea kusaidia shughuli za kijamii - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, October 4, 2017

Tanga Cement yazidi kujitolea kusaidia shughuli za kijamii

Meneja Usambazaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Samuel Shoo, akikabidhi msaada sehemu ya mifuko 500 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 6  kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Rehema Said (kulia), iliyotolewa kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Majengo iliyomo wilayani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika eneo la kiwanda cha TCPLC, Pongwe, Tanga hivi karibuni. Wengine pichani ni maofisa wa Saruji Tanga na kutoka Korogwe.

Meneja Ubora wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Michael Ruzige (kushoto), akikabidhi msaada wa sehemu ya mifuko 100 ya saruji kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mlalo, Catherine Freedom iliyotolewa kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Ngazi iliyopo Mlalo wilayani Lushoto. Hafla ya makabidhiano ilifanyika eneo la kiwanda cha TCPLC, Pongwe, Tanga hivi karibuni. Wengine ni wafanyakazi wa Saruji na wa kutoka Mlalo.

Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Nje wa kampuni ya Saruji Tanga, Bi. Mtanga Noor (kushoto), akikabidhi msaada waa mifuko 500 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 6  kwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Mji wa Korogwe, Jumanne Shauri ( (kulia), iliyotolewa kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Majengo iliyomo wilayani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika eneo la kiwanda cha TCPLC, Pongwe, Tanga hivi karibuni. Wengine pichani ni maofisa wa Saruji Tanga na kutoka Korogwe.

Mkurugenzi wa Halamashauri ya Mji wa Korogwe, Jumanne Shauri (aliyevaa koti katikati), akizungumza na akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kupokea  msaada wa mifuko 500 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 6 iliyotolewa na Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), kusaidia ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Majengo iliyopo wilayani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika eneo la kiwanda cha TCPLC, Pongwe, Tanga hivi karibuni. Kulia kwake ni Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Nje wa kampuni hiyo, Bi. Mtanga Noor baadhi ya wafanyakazi na wawakilishi kutoka Korogwe.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Dk. Elizabeth Nyema (wa nne kulia), akizungumza na akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kupokea  msaada wa mifuko 500 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shs milioni 6 iliyotolewa na Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), kusaidia ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Majengo iliyopo wilayani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika eneo la kiwanda cha TCPLC, Pongwe, Tanga hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages