RC MAKALLA: HITILAFU YA UMEME CHANZO CHA KUUNGUA SOKO LA VETERINARY - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Monday, May 30, 2022

demo-image

RC MAKALLA: HITILAFU YA UMEME CHANZO CHA KUUNGUA SOKO LA VETERINARY

18baa5a6-9458-4f1b-8c73-aef521958030
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam . Amos Makalla, akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo soko limeungua
cf3f91ce-75a4-4412-ac41-ce7c58a9f3ab
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akiawa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Jokate Mwegelo na viongozi mbalimbali eneo ambapo soko limeungua Vetenari wilayani Temeke.
1fd9de82-8804-434a-82ee-cb6fa4c0e96b
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla, akionyesha baadhi ya mejengo yalioanguka kutokana na moto huo.
d104abe3-0f9a-446a-92ca-22990d78ae0f
f9891b6f-4b27-45fe-90af-82f07eab0301
- Asema kazi ya kurejebisha Miundombinu iliyoungua itafanyika usiku na mchana.

- Awahakikishia Wafanyabiashara hakuna atakaehamishwa.

- Asisitiza Masoko kuwa na Fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO.

- Aonya tabia ya Mamalishe kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema chanzo Cha Moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ilitokana na Hitilafu ya umeme.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko Hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453.

Aidha RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha Miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na Biashara Kama awali ambapo ameahidi hakuna mfanyabiashara atakaeondolewa.

Hata hivyo RC Makalla ametoa pole kwa Wafanyabiashara walioathiriwa na Moto huo na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali yao inaendelea kutatua changamoto hiyo.

Kutokana na matukio ya Moto kujirudia Mara kwa Mara, RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO, Halmashauri kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye Kila soko, Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva huku akisisitiza Masoko kuwa na Ulinzi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *