Wanariadha wa mbio za ndani na kimataifa wa mbio za masafa na fupi wameendelea kujinoa tayari kwa ajili ya michuano za kimataifa duniani maarufu Kilimanjaro marathon 2025 ikiwa ni msimu wa 23 wa mbio hizo nchini.
Mikoa ya kaskazini ikiwemo Arusha inatajwa kuwa na wanariadha wengi ambao wamekuwa wakifanya vyema katika mashindano ya kimataifa, kutana na bingwa mtetezi wa mbio za kilometa 21 zinazo dhaminiwa na kampuni Chapa Yas na Mix by Yas, Faraja Lazaro, anaeleza umuhimu wa michuano hiyo katika kuongeza thamani sekta ya michezo na wachezaji wa riadha Tanzania.
-Faraja Lazaro-Bingwa Mtetezi wa 21 Km mwaka 2024.
-Elibariki Zephania-Mwanariadha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Yas Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo amesema maandalizi kuelekea mashindano hayo yamekamilika na kuwataka wananchi wakiwemo wanariadha kujitokeza kwa wingi na kufanya vizuri katika michuano hiyo huku huduma za mawasiliano chini ya udhamini wa Yas na Mixx by Yas zikiwa zimeimarishwa kwa wageni na wafanyabiashara.
-Henry Kinabo-Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kaskazini.
Kocha Andrew Panga ni miongoni mwa wakufunzi wa mchezo wa riadha Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha amesema muamko wa wanariadha wengi umekuwa juu na hamasa tayari kwa ajili ya kuoneshana undava na wanariadha wageni watakaoshiriki mashindano hayo ikiwa ni mwaka wa 10 Yas wanadhamini nusu marathon mwaka huu.
-Andrew Panga-Kocha wa mchezo wa Riadha Tanzania.
Michuano hiyo inatarajiwa kutimua vumbi Februari 23/2025, mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania ambapo zaidi ya washiriki 2000 wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo wakiwemo watalii kutoka mataifa mbalimbali Duniani.
No comments:
Post a Comment