Wasanii na vikundi vinavyopiga muziki wa bendi wametakiwa kujitazama upya juu ya muziki huo kutumika kama chombo cha kuuzia bia kwenye Bar.
Hayo yamesemwa na msanii nguli wa muziki wa dansi hapa nchini John Kitime alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la sanaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa nchini (BASATA).
“kuna vitu tunafanya tunaona kama vya kawaida lakini ndio vinaua muziki wetu kama leo hii, bendi zinapiga kwenye bar kwa ajili ya kuuza bia na watu wanaangalia bure, hivyo inamaanisha bendi zetu ndio kichocheo cha kuuza pombe katika mabaa yote mjini” amesema Kitime.
Kitime ametoa wito kwa wasanii kuanza kubadilisha mtindo wa maisha kwani kitendo cha bendi zote kuhamia kwenye bar ni moja ya anguko kubwa la muziki wa dansi nchini.
No comments:
Post a Comment