SIASA: Sasa Huenda Gobdless Lema Akaachiwa kwa Dhamana - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, February 27, 2017

SIASA: Sasa Huenda Gobdless Lema Akaachiwa kwa Dhamana

ARUSHA: Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ikiongozwa na majaji watatu, iliyokaa Arusha leo Februari 27, 2017 imetupilia mbali Rufaa zote mbili zilizofunguliwa na Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuhusu pingamizi la dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema.
Wakili wa Lema, Peter Kibatala amesema kuwa tangu awali waliwaambia serikali kuwa rufaa hizo mbili walizozifungua dhidi maamuzi ya mahakama kuu kuwa hazikuwa na mantiki yoyote kisheria.
Hata hivyo, mahakama hiyo imetoa maelekezo kuwa jalada la kesi hiyo lipelekwe Mahakama Kuu ili kuendelea na mchakato wa kumpatia dhamana katika kesi inayomkabili kwani hakuna hoja ya msingi kwa rufaa iliyokatwa na mawakili wa serikali.
Majaji wamesema wamesoma mapingamizi ya mawakili wa serikali bila kuona tija yoyote ya kisheria kwa hiyo imetoa amri kwa Mahakama Kuu kulishughulikia suala la Godbless Lema haraka.
Mbunge huyo aliyekamatwa Novemba 2 mwaka jana, mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Dar kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi, amesota rumande kwa takribani miezi minne sasa na leo amerejeshwa tena rumande baada ya mahakama kuamuru kesi yake iriejeshwe kwenye mahakama zinazoweza kumpatia dhamana.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema akiwasili mahakamani leo.


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Mbunge wa Kibamba wakiwasili katika Mahakama ya Rufani Arusha Leo, Jumatatu 27/02/2017 kusikiliza shauri la Mbunge Godbless Lema.

Viongozi wengine waliofika mahakamani leo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Mwesiga Baregu, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro, Katibu wa CHADEMA Arusha, Aman Golugwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages