Siku moja mara baada ya kuwasili nchini akiwa na tuzo ya MTV base msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba, ameondoka nchini kwenda Marekani kwa ajili ya maonyesho yake ya kimuziki katika nchi hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa Wor'Out Media, mdogo wa msanii huyo Abdul Kiba amesema kuwa kiba amerudi nchini kwa ajili ya kuleta tuzo ya MTV kwa Watanzania na hivyo kesho jioni tunaondoka kwenda marekani.
“tunaondoka kwenda marekani na tutafanya maonyesho matano katika miji tofauti ya nchi hiyo hivyo mashabiki wetu waendele kutegemea kupata makubwa kutoka kwetu” amesema Abdul Kiba.
Amesema kuwa kwa sasa ratiba yao ipo taiti katika kufanya maonyesho ya kimataifa na wakirejea watafanya kitu kikubwa kwa watanzania na Afrika kwa ujumla.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba
No comments:
Post a Comment